Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecil David Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, kweli kuna wazee wanaodai haki zao kutokana na ushiriki wao kwenye Vita vya Dunia au Jeshi la KAR?
Supplementary Question 1
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, Vita ya Pili ya Dunia ilikwisha mwaka 1945 na wapiganaji Tanzania walikuwa 680 na sasa wamebakia 58 maana yake wanazidi kuisha na Serikali haijafanya uhakiki ili waweze kulipwa fidia ama kurejeshewa mali zao nataka nifahamu ni lini Serikali itamaliza zoezi la uhakiki ili hawa watu waweze kupata stahiki zao? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kulikuwa na Vita ya Kagera pia hapa Tanzania waathirika wa Vita ya Kagera pamoja na Wanajeshi Wastaafu wako mtaani, kila mara wamekuwa wanakwenda kwenye Ofisi za Wilaya kujiandikisha wakiamini kwamba wanastahili kupata stahiki zao lakini pia pamoja na pensheni na matibabu. Ni lini Serikali itakamilisha taratibu hizi ili hawa watu wetu ambao ni wazalendo waweze kupata haki zao za msingi? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, kuhusu lini tutamaliza zoezi hili naamini muda si mrefu kwa sababu awali tulikuwa tunawasiliana na Serikali ya Uingereza, baadaye tukabaini kwamba KAR hawa taarifa zao zilikuwa makao makuu ya wakati huo Nairobi, sasa hivi Wizara yetu ya Mambo ya Nje inawasiliana na wenzetu wa Kenya ili kupata taarifa hizo na kwa sababu kwa sasa waliopo ni wachache tunaamini baada ya miezi miwili tutakuwa tumepata taarifa hizi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu hawa wa Vita ya Kagera tumeshajibu swali kama hili huko nyuma ni kwamba baada ya Vita ya Kagera askari waliokuwa na sifa ya kuendelea kubaki jeshini waliajiriwa na wale ambao walikosa sifa walilipwa malipo yao ya mkupuo na kutakiwa kurudi nyumbanI, lakini tumebaini kwamba majemedari wetu hawa baadhi yao wameendelea kuwa na changamoto za kiafya na hivyo Serikali ikakubali kuanza kuwahudumia kwenye Hospitali za Jeshi zilizo karibu na wao.
Mheshimiwa Spika, suala la pensheni lilishindikana kwa sababu kwa vigezo vya ajira hawakukidhi na hivyo ilikuwa ni vigumu kuwaingiza kwenye utaratibu wa pensheni, nashukuru (Makofi)
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, kweli kuna wazee wanaodai haki zao kutokana na ushiriki wao kwenye Vita vya Dunia au Jeshi la KAR?
Supplementary Question 2
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na tunashukuru sana swali hili lilivyoulizwa mara ya mwisho ulitoa maelekezo kwamba wazee hawa washughulikiwe kwa haraka sana. Sasa Njombe wazee hawa wamefuata utaratibu wamekwenda kuripoti lakini bado wanasumbuliwa sana, tunaomba tuelewe hasa ni lini jambo hili litakamilika?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, kama anakusudia wazee wa KAR hawa 58 taarifa zao tunazo, uhakiki uliokuwa unafanyika ni kuthibitisha pasipo na shaka mali zao wanazostahiki ni zipi. Hadi sasa taarifa zinaonyesha karibu mali zilizopatikana zilizokuwa na utata ni za shilingi bilioni 15, kwa hivyo mara utakapo kamilisha kama nilivyosema wazee hawa watalipwa.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kama nawalenga wazee wa Kagera nimeshaeleza utaratibu uliopo kama kuna watu ambao kwa bahati mbaya wanaona hawakufikiwa wawasiliane na Kambi za Jeshi zilizo karibu na maeneo yao au Ofisi za Wakuu wa Wilaya ili taarifa zao ziweze kuchukuliwa na huduma stahiki ziweze kutolewa.
Mheshimiwa Spika, nashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved