Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 10 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 119 2024-04-19

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. COSATO D. CHUMI K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Nsanga – Kiteputepu katika Kata ya Ntaba – Busokelo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Daraja la Nsanga linaunganisha Kata ya Ntaba upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo na Kata ya Ipinda upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela. Daraja hilo hutumiwa na wakulima wa mpunga na kokoa kutoka mashambani kwenda kwenye masoko.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali kupitia TARURA imetenga shillingi 500,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu la zege katika sehemu hiyo ambapo kwa sasa kuna kivuko cha waenda kwa miguu ambacho kinatumika.