Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 10 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 120 2024-04-19

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza kutumia wataalam wa ujenzi kwenye Miradi ya Force Account hata ikiwa kwa mikataba?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inazingatia miongozo iliyopo kwenye kutekeleza kazi za ujenzi wa miradi kwa kutumia njia ya force account ili miradi hiyo iweze kutekelezwa kwa ubora na ufanisi mkubwa. Aidha, Serikali imekua ikiwatumia wataalamu wa ujenzi kwa mikataba na waajiriwa wa halmashauri ili kuhakikisha miradi inayojengwa kwa force account inakua bora na imara.