Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza kutumia wataalam wa ujenzi kwenye Miradi ya Force Account hata ikiwa kwa mikataba?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, je, Serikali sasa haioni kuwa kuna haja ya kutumia wahitimu waliohitimu ufundi katika Miradi ya Force Account?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Serikali haioni kuwa, kuna haja ya kushirikiana na taasisi za ufundi ili kusimamia miradi ya force account badala ya kutumia watumishi ambao hawana fani hizo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, tunapokea mawazo ya Mheshimiwa Mbunge, tutachakata maoni yake na tuone tunaweza vipi kuboresha ufanisi katika utekelezaji wa miradi hii.