Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 10 Community Development, Gender and Children Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 126 2024-04-19

Name

Dr. David Mathayo David

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Same Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kumwelimisha mtoto wa kiume kujitegemea, kujiamini na kufahamu majukumu ya baba wa familia pindi anapooa?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imeandaa Mwongozo wa Wajibu wa Wazazi katika Malezi ya Watoto kwa kuzingatia jinsi ambavyo inajumuika kama Familia Bora, Taifa Imara, wenye lengo la kuimarisha ushiriki wa wazazi na walezi katika malezi ya watoto. Moja ya eneo lililoainishwa katika mwongozo huo ni kumwandaa mtoto wa kiume ili aweze kumudu majukumu ya baba katika nyanja tofauti ikiwa ni pamoja na kutambua wajibu na nafasi katika malezi ya watoto na familia, ahsante.