Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 10 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 131 2024-04-19

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Malambo ya kunyweshea mifugo katika Jimbo la Meatu?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa bwawa/lambo hufanyika kwa hatua tatu ambazo ni kutafuta chanzo cha maji (water source), kufanya usanifu (design) na kutekeleza kazi ya ujenzi. Wizara itawasiliana na Halmashauri ya Wilaya Meatu kwa ajili ya kupata mapendekezo ya eneo linalofaa kujenga lambo ambalo halina mgogoro wa umiliki, ili hatua za usanifu ziweze kufanyika na kuingiza gharama zake kwenye Mpango wa Bajeti ya Wizara kadiri ya upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia kutoa wito kwa wafugaji na wadau wengine hapa nchini kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya maji ili kusaidia kupunguza changamoto ya maji kwa ajili ya mifugo. Naomba kuwasilisha. (Makofi)