Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Malambo ya kunyweshea mifugo katika Jimbo la Meatu?

Supplementary Question 1

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali haioni haja kwenye mabwawa saba yaliyotengwa katika Mradi wa ASDP II ukiwemo Mkoa wa Simiyu, likajengwa katika Jimbo la Meatu kwa sababu ndio wilaya yenye mifugo mingi, ndio wilaya yenye ukame mkubwa na maeneo yapo mengi, wafugaji wapo tayari kuyatoa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; je, ni lini Serikali itakipelekea shilingi milioni 6.8 Kikundi cha Mwamalole cha kupanda nyasi kwa kuwa, mvua nazo zinaeleka kwisha? Nakushukuru. (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, naanza na hili la kwanza la mabwawa saba; tumepokea maombi ya Mheshimiwa Mbunge na ushauri wake. Tutatazama tuone namna ambayo inafaa zaidi kwenye Jimbo lake hili la Meatu. Kwa kuongezea katika hilo ni kwamba, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Kilimo pamoja na Wizara ya Maji tumekubaliana yale malambo yanayojengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo cha uwagiliaji ambayo yanajengwa na Wizara ya Kilimo pamoja na mabwawa makubwa yanayojengwa na Wizara ya Maji ambayo yanafanya shughuli za kuhifadhi maji, tumekubaliana sasa yawe na mabirika kwa ajili ya wafugaji ili yaweze kutumika kwa shughuli za mifugo katika maeneo yetu. Kwa hiyo, tutaangalia katika malambo saba ambayo yanajengwa na pia, tutaangalia katika Wizara ya Kilimo na Wizara ya Maji, kama kuna uwezekano wa kutengeneza mabirika kwa ajili ya wafugaji wetu ili waweze kupata huduma hiyo ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili la pili, la shilingi milioni sita kwenda kwa vikundi vyake. Namwomba Mheshimiwa Mbunge kwamba, leo nitalifuatilia jambo hili na baada ya hapo nitakupa majibu halisi juu ya namna gani ambayo tunakwenda kusaidia vikundi vyetu hivyo katika maeneo yetu. Ahsante. (Makofi)