Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 10 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 132 2024-04-19

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha Skimu ya Umwagiliaji ya Rwamfi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Rwamfi, Katongolo, ni Skimu ya Umwagiliaji ambayo ipo katika Kata ya Kirando na Kipili, Tarafa ya Kirando katika Wilaya ya Nkansi, Mkoani Rukwa. Skimu hii ina eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta 3,300 na inahudumia jumla ya vijiji sita kikiwemo Kijiji cha Masolo, Katongolo, Kipili, Mtakuja, Kamwanda na Katete.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilikamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu hiyo kwa lengo la kuiboresha kwa kufanya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji. Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Mkandarasi Halem Construction Company Limited amepatikana na mkataba unategemewa kusainiwa mwishoni mwa Mwezi Aprili, 2024 kwa ajili ya kuanza ukarabati na ujenzi. (Makofi)