Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 11 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 133 2024-04-22

Name

Angelina Adam Malembeka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuongeza posho kwa Askari na Maafisa Wasimamizi wa Uchaguzi?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, wakati wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Ngazi ya Jimbo na Kata hulipwa posho za kujikimu wanapokuwa wanatekeleza majukumu ya uchaguzi kwa kuzingatia Waraka wa Utumishi wa Umma kuhusiana na posho za Serikali. Kwa sasa Serikali imefanya maboresho kwa kuongeza viwango vya posho hizo kupitia Waraka wa Utumishi wa Umma Na.1 uliotolewa tarehe 24 Mei, 2022.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Watendaji na Walinzi wa Vituo vya Kupigia Kura, utaratibu wa uboreshaji wa viwango vyao vya posho utazingatiwa wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, ahsante.