Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 11 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 134 2024-04-22

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuunga mkono juhudi za wananchi wa Kata ya Mbebe kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya vilivyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi sambamba na kujenga vituo vipya.

Mheshimiwa Spika, Boma la Kituo cha Afya Kata ya Mbebe limejengwa kwenye Zahanati ya Mbebe ambapo eneo lina ukubwa wa ekari tatu. Eneo hilo halitoshi kwa ujenzi wa kituo cha afya. Hivyo, Halmashauri inapaswa kutafuta eneo litakalowezesha ujenzi wa kituo cha afya wakati Serikali ikiendela kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi, ahsante.