Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 11 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 138 2024-04-22

Name

Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER E. MALLEKO K.n.y. MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: -
Je, Serikali imefikia wapi kuweka utaratibu rahisi wa urasimishaji na umilikishaji ardhi hususani kwa Wanawake?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mradi wa kuboresha usalama wa miliki za ardhi kupitia mradi wa (LTIP) kwa mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia ambayo unafanyika katika mamlaka za upangaji 58 nchini. Kupitia mradi huo, haki za wanawake zimezingatiwa ipasavyo katika utoaji wa elimu na uhamasishaji umiliki wa ardhi kwa wanawake na umiliki wa pamoja baina ya mume na mke.

Mheshimiwa Spika, kupitia utaratibu huo, vikosi kazi vimeundwa kwa ajili ya kushughulikia uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa makundi maalum ya wanawake, wazee na walemavu katika suala la urasimishaji makazi pamoja na umiliki wa pamoja wa ardhi. Aidha, elimu inatolewa kupitia vyama vya hiari vya kijamii, mashirika yasiyo ya Kiserikali; CSO’s na NGO’s ambapo mikutano ya elimu kwa umma kuhusu utekelezaji wa miradi imefanyika katika ngazi za Mitaa, Kata na Wilaya. Jumla ya wananchi 3,249 wamehudhuria mikutano hiyo wakiwemo wanaume 1,518 na wanawake 1,731.

Mheshimiwa Spika, mradi pia umewezesha kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi nchini kutoka 25% hadi 41%. Vilevile idadi ya hatimiliki za pamoja (joint titles) kati ya wanandoa zimeongezeka na kufika 10% ya hati zinazotolewa.