Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 52 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 458 2022-06-27

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Primary Question

MHE. HAMISI M. MWINJUMA aliuliza:

Je, kuna mpango gani kuruhusu watu/taasisi binafsi hasa za wasanii kukusanya mirabaha maeneo ya wazi yanayotumia kazi za sanaa?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamisi Mohamed Mwinjuma, Mbunge wa Muheza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango wa kuruhusu watu binafsi na Taasisi kuanza kukusanya mirabaha na tayari mapendekezo yameshaletwa kwenye Financial Bill ya mwaka 2022. Aidha, inapendekezwa COSOTA kubaki na jukumu la kusimamia Hakimiliki na jukumu la ukusanyaji na ugawaji wa Mirabaha kwenda kwa Taasisi au Wadau binafsi yanii Collective Management Organizations (CMOs). Nakushukuru.