Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Primary Question

MHE. HAMISI M. MWINJUMA aliuliza: Je, kuna mpango gani kuruhusu watu/taasisi binafsi hasa za wasanii kukusanya mirabaha maeneo ya wazi yanayotumia kazi za sanaa?

Supplementary Question 1

MHE. HAMISI M. MWINJUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na nashukuru kwa majibu ya kutia moyo ya Serikali. Na nina swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa vile suala hili linakuja na maslahi makubwa ya kiuchumi na kuna Ushahidi wa migongano katika maeneo kadhaa ambayo CMOs zimewahi kuruhusiwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha migogoro miongoni mwa CMOs hizi binafsi haitakuwepo?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika, nikushukuru. Naomba nijibu swali la nyongeza moja la Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma, Mbunge wa Muheza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Sheria hii ilipoanza kutekelezwa kwenye nchi zingine kuna migogoro ilijitokeza baina ya wadau. Sisi tumejipanga baada ya hili kupitishwa na Bunge hili tutakaa na wadau wote wa tasnia mbalimbali katika sanaa, kama ni wanamuziki wa Injili, kama ni wanamuziki wa Kizazi Kipya tutakaa nao. Tutahakikisha Uongozi wao tunauimarisha, lakini pia wanafahamu kwa nini CMOs zikakusanye na COSOTA itasimamia suala zima, kuhakikisha kwamba hawa watu hawaingii kwenye mgogoro.