Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 52 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 459 2022-06-27

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga majengo mapya ya kisasa ya Mahakama ya Wilaya Hai kwa kuwa jengo la sasa ni chakavu?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipeleka wataalam na kubaini kuwa ni kweli Mahakama ya Hai ni chakavu na hivyo ilihitaji ukarabati. Ukarabati katika Mahakama hii ulishafanyika toka Februari, 2021.