Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 14 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 185 | 2024-04-25 |
Name
Edwin Enosy Swalle
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupembe
Primary Question
MHE. EDWIN E. SWALLE aliuliza:-
Je, lini Serikali itarejesha Kiwanda cha Chai cha Wakulima wa Lupembe, Muvyulu?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kuanzia Mwezi Januari, 2024, Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina ilianza kufanya tathmini ya mali za Kiwanda cha Chai cha Wakulima, Lupembe, kwa ajili ya kumlipa mwekezaji (Dhow Mercantile East Africa Limited) fidia kulingana na thamani halisi ya mali za kiwanda kabla ya kukirejesha kwa Wakulima wa Lupembe (MUVYULU). Kazi hiyo ya tathmini inatarajiwa kukamilika kabla ya Mwezi Juni, 2024.
Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa kazi hiyo kutawezesha mwekezaji huyo kulipwa fidia kulingana na makubaliano yaliyofikiwa baina ya mwekezaji huyo na Chama cha Ushirika cha Muvyulu ambapo Serikali itarejesha kiwanda hicho kwa wakulima wa zao la chai, Lupembe.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved