Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Edwin Enosy Swalle
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupembe
Primary Question
MHE. EDWIN E. SWALLE aliuliza:- Je, lini Serikali itarejesha Kiwanda cha Chai cha Wakulima wa Lupembe, Muvyulu?
Supplementary Question 1
MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kuishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa kumaliza huu mgogoro wa Kiwanda cha Lupembe ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Kwa hivyo, sasa hivi tuko hatua ya mwisho, ni hatua nzuri kwa Serikali, hongera sana Mheshimiwa Dkt. Samia.
Mheshimiwa Spika, ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza kwenye majibu ya Mheshimiwa Waziri. Swali la kwanza; kwa kuwa, kiwanda hiki ni kiwanda cha muda mrefu cha tangu mwaka 1958 mpaka leo, kwa hiyo, mitambo mingi imechakaa. Je, kitakaporejeshwa kwa wananchi, Serikali iko tayari kuwakopesha Wakulima wa Chai, Lupembe, fedha kupitia Mfuko wa Kilimo ili waendeshe kiwanda hiki?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa, Wakulima wa Chai Lupembe, baadhi wana madai kwa mwekezaji na wapo baadhi ya wafanyabiashara, pia wana madai kwa mwekezaji na mwekezaji huyu anakusudia kuondoka baada ya kulipwa fidia. Je, ni nini Kauli ya Serikali kwenye madeni ya wakulima ambao hawajalipwa? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, baada ya kiwanda kurudishwa kwa wananchi, Serikali itakuwa tayari kutoa mkopo kupitia Benki ya TADB ili kuweza kukifufua kwa kuweka mitambo mipya ili kiweze kufanya kazi kwa ukamilifu zaidi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu madai kwamba, sehemu ya tathmini inayofanyika kabla ya kumlipa maana yake unapofanya tathmini ni pamoja na kuangalia madeni ambayo wanalipwa, kwa hiyo, itakuwa ni sehemu ya huo mchakato mzima. Kwa hiyo, wananchi watalipwa kabla ya kiwanda hiki kurejeshwa kwa wakulima, ahsante.
Name
Timotheo Paul Mnzava
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Vijijini
Primary Question
MHE. EDWIN E. SWALLE aliuliza:- Je, lini Serikali itarejesha Kiwanda cha Chai cha Wakulima wa Lupembe, Muvyulu?
Supplementary Question 2
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, kwa zaidi ya miezi miwili sasa Viwanda vya Chai vya Ambangulu na Dindira vimefungwa na wananchi hawana maeneo ya kupeleka chai. Ni nini Kauli ya Serikali kuwasaidia wananchi hawa, ili waweze kuendelea na shughuli zao za kilimo na uzalishaji? Nakushukuru.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli tunafahamu changamoto ambayo Mheshimiwa Mbunge ameieleza na kwamba, Wizara ya Kilimo tumeshawaandikia wawekezaji wote akiwemo mmiliki wa Kampuni ya Mohamed Enterprise kwanza kufungua hicho kiwanda.
Mheshimiwa Spika, pili, tunaendelea na mazungumzo kama ambayo tunafanya katika Halmashauri ya Lupembe kuhakikisha kama ameshindwa uendeshaji. Maana yake viwanda hivi sisi kama Serikali tutakuwa tayari kumlipa fidia ili kuvirejesha kwa wananchi ili waweze kuviendesha wenyewe kupitia vyama vya ushirika. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved