Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 39 2024-04-05

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza:-

Je, upi mpango wa Serikali wa kujenga barabara na mitaro Geita Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024, Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 77.94 na ujenzi wa mitaro yenye jumla ya kilometa 6.395. Aidha, Geita ni miongoni mwa miji 45 inayotekeleza Mradi wa Kuboresha Miundombinu Shindanishi katika Miji Tanzania (TACTIC) ambapo mradi utajenga kilometa 17 za barabara kwa kiwango cha lami na kilometa 25 za mitaro kwa gharama ya shilingi bilioni 22.23.