Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 546 2024-06-06

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Boma, Kijiji cha Doma, Wilayani Mvomero?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu;-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Doma kipo Kata ya Doma, Kijiji cha Doma katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero. Ujenzi wa kituo hiki ulianza mwaka 2021/2022 kwa wananchi kuanza ujenzi wa jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD) ambalo limefikia hatua ya kupandisha kuta.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imetenga shilingi milioni 40 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo hilo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya cha Doma.