Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 15 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 188 2024-04-29

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question


MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kijiji cha Koresa, Kata ya Vunjo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua mahitaji ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati kote nchini. Aidha, Serikali inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi viporo pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vipya kwenye maeneo ya kimkakati ikiwemo Kituo cha Afya cha Koresa katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa wananchi wa Kijiji cha Koresa wanapata huduma za afya kwenye Kituo cha Afya cha Himo. Ahsante.