Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 15 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 189 2024-04-29

Name

Salim Alaudin Hasham

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulanga

Primary Question

MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Hospitali mpya ya Wilaya ya Ulanga?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ilianza kutoa huduma mwaka 1905 kama Kituo cha Afya na baadaye kupandishwa hadhi na kuwa Hospitali. Aidha, hospitali hii ni miongoni mwa hospitali kongwe 50 ambazo Serikali ilizifanyia tathmini, kwa ajili ya ukarabati mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imetenga shilingi bilioni 27.9 za ukarabati wa hospitali kongwe 31 zilizobaki ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Ulanga, ambayo imepokea shilingi milioni 900 ambapo ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali unaendelea, ahsante.