Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 15 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 193 2024-04-29

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kijiji cha Msufini Kata ya Hembeti Mvomero?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Skimu ya Umwagiliaji ya Msufini yenye jumla ya hekta 1,000 iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero inakabiliwa na changamoto ya banio kuachwa na mto ambao ndiyo chanzo chake kikuu cha maji sambamba na mchanga kujaa kwenye mto huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Mradi wa Msufini ili kujua gharama halisi za utekelezaji wa mradi huu na miundombinu sahihi itakayohitajika ili kukabiliana na changamoto zilizopo sasa. Aidha, kukamilika kwa ujenzi wa skimu hii utanufaisha wakulima 320