Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kijiji cha Msufini Kata ya Hembeti Mvomero?

Supplementary Question 1

MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa tuna skimu za umwagiliaji ambazo ujenzi wake ulianza muda mrefu sana na skimu hizi hazifanyi kazi ikiwemo Skimu ya Lukenge ambayo ina wakulima zaidi ya 3,000 na Skimu ya Luhindo ina wakulima zaidi ya 2,400; tarehe 25 Machi, mlitangaza tender ya kumpata mzabuni wa kununua pampu mbili kwa ajili ya kwenda kufunga kwenye hizi skimu. Je, ni lini Serikali itakamilisha kazi ya kutafuta hizi pampu na kwenda kufunga ili skimu hizi ziweze kufanya kazi na kuwasaidia wakulima wetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Kata ya Mlali, Kijiji cha Mlali tuna skimu ambayo inajiendesha kienyeji, ina wakulima zaidi ya 400 na ni skimu ambayo ina hekta zaidi ya 500. Je, Serikali haioni sasa ni wakati mwafaka wa kuwatuma wataalamu wa umwagiliaji kwenda kufanya tathmini ili skimu hii iweze kupanda hadhi na iweze kupangiwa bajeti ili kuiboresha hii skimu.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba katika Skimu za Lukenge na Ludigo ambapo tuliweka pampu katika tenda na zimeshafika mkoani, ninachomwagiza tu RM wa Mkoa wa Morogoro ni kuzipeleka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ambayo ilichelewesha ni hizi mvua zilizokuwa zimezidi sana, ndiyo maana walishindwa kupeleka, kwa sababu unaweza kupeleka halafu vikaharibika tena. Kwa hiyo, kwa sababu mvua zinaendelea kupungua, maana yake tutaendelea kuzikamilisha ili wananchi waweze kupata huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Skimu ya Mlali, tutawatuma wataalamu ili waende pale wakafanye tathmini na upembuzi yakinifu ili watuletee gharama halisi na kuijenga kisasa ili mradi uweze kutumika kwa wananchi wote, ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kijiji cha Msufini Kata ya Hembeti Mvomero?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa hii nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tuna Skimu ya Mbwasa na Skimu ya Udimaa ambazo tayari Serikali ilishafanya upembuzi yakinifu. Je, ni lini sasa Serikali itatangaza tenda za ujenzi wa hizi skimu mbili? Ahsante.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba skimu zote mbili ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja ikiwemo ya Mbwasa zipo katika mchakato wa kumtafuta mkandarasi hivi sasa tunavyozungumza. Kwa hiyo, mchakato ukishaisha, maana yake sasa tutasaini mkataba ili zianze ujenzi wake, ahsante.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kijiji cha Msufini Kata ya Hembeti Mvomero?

Supplementary Question 3

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya Serikali tunayoimalizia ilitenga fedha za feasibility study na ujenzi wa Skimu za Netrom, Makeresho, Bolutu, Kikafu Chini, Mwera, Kalali, Bwana Mganga, Mtambo, Ismail, Longoi, Mapacha pamoja na ujenzi wa common using facilities. Je, ni lini sasa Serikali itaanza feasibility study na ujenzi wa miradi hii?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba mchakato wa feasibility study unaendelea, nikuhakikishie tu kwamba miradi yote ambayo tuliiweka katika bajeti, washauri elekezi wametafutwa kwa ajili ya hiyo kazi ambayo inafanywa sasa hivi. Kwa hiyo, nikuondoe shaka tu kwamba watu wa Makeresho watapata huduma yao pamoja na maeneo mengine yote uliyoyataja, ahsante.

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kijiji cha Msufini Kata ya Hembeti Mvomero?

Supplementary Question 4

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Skimu ya Umwagiliaji ya Ruaha Mbuyuni imebomoka kwa muda mrefu sasa na inawahudumia wananchi zaidi ya 10,000 pale. Ni mpango gani wa Serikali kuhakikisha kwamba ukarabati wa haraka unafanyika ili wale wananchi waendelee kunufaika na shughuli zao za kilimo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua changamoto ya Skimu ya Ruaha Mbuyuni na tutairekebisha haraka iwezekanavyo. Changamoto kubwa zilikuwa ni hizi mvua ambazo zilikuwa zinaendelea. Kwa hiyo, hatuwezi kuiacha kwa sababu tunajua umuhimu wa hii skimu, ahsante.