Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 48 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 423 | 2022-06-21 |
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Primary Question
MHE. DEUS C. SANGU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela, kama ifuatavyo: -
Mheshimwa Naibu Spika, Sera ya Serikali ni kujenga Vyuo vya VETA katika kila Wilaya nchini na siyo katika Halmashauri. Aidha, katika Mkoa wa Rukwa Serikali inaendelea na ujenzi wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa katika Wilaya ya Sumbawanga ambapo wanufaika wa Chuo hicho ni pamoja na wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved