Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 5 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 55 2024-04-08

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kununua Jenereta katika Hospitali ya Ilongero na Vituo vya Afya Mgori, Makuro na Msange - Jimbo la Singida Kaskazini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida Ilongero pamoja na Kituo cha Afya Msange vimeshapokea jenereta kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na taratibu za ufungaji zinaendelea. Kituo cha Afya Mgori kitapokea mgao wa jenereta katika Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Singida itatenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa jenereta la Kituo cha Afya Makuro.