Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 5 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 82 | 2024-09-02 |
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Mahakama za Mwanzo za Sanza na Kintinku?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Chaya kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Mahakama ya Tanzania inaendelea kutekeleza mpango wake wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama kwa mwaka 2021/2022 – 2025/2026 katika ngazi mbalimbali za Mahakama. Kutokana na uhaba wa majengo ya Mahakama, majengo haya yanajengwa na kukarabatiwa kwa awamu kwa kuzingatia mpango huo na kadri fedha zinavyopatikana.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango huu unatarajia kukamilika mwaka 2025/2026 na sasa hatua za kuuhuisha zinaendelea ambapo majengo ya Mahakama ya Mwanzo Sanza na Kintinku yatajumuishwa katika mpango huo. Nashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved