Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Mahakama za Mwanzo za Sanza na Kintinku?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tunafahamu wananchi wanapata adha kubwa sana ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma za Mahakama katika Makao Makuu ya Wilaya na kwa kuwa tuna uhaba wa Mahakama za Mwanzo, nini mkakati wa Serikali wa kuweka mifumo ya TEHAMA katika Mahakama za Mwanzo ili kupunguza adha ya kusafiri na kutumia gharama kubwa wananchi?
Mheshimiwa Naibu Spika, Swali la pili, kwa kuwa mpango wa kujenga Mahakama za Mwanzo utaanza mwakani kama alivyotangulia kusema Mheshimiwa Naibu Waziri, nini sasa mkakati wa Serikali wa kutumia mobile court (Mahakama Tembezi) kwa maeneo ambayo ni hard to reach ili tuwawezeshe wananchi wanaokaa maeneo ya mbali waweze kupata hii huduma? Ahsante sana.
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu umuhimu wa kuweka TEHAMA katika Mahakama za Mwanzo, nakiri kwamba hiyo hali ndiyo mwelekeo wetu wa Idara yetu ya Mahakama ambapo kwa Mahakama za Mwanzo zilizopo katika miji kwa maana mijini kama Primary Courts in the cities na kwenye municipalities tayari wameshaunga na mfumo wa TEHAMA, lakini kule vijijini changamoto tunayokutanayo ni kwamba Mkongo wa Taifa haujafika kwenye maeneo yale, kwa hiyo, kadri Serikali inavyoendelea kupanua huduma za Mkongo wa Taifa na umeme vijijini na kuzifikia sehemu zenye Mahakama za Mwanzo, Mahakama pia zitaingiza utaratibu wa TEHAMA ili kuwarahisishia wananchi kufanya mawasiliano na Mahakama.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mobile courts, tunatambua kwamba yapo maeneo kweli ni makubwa na hayana majengo ya Mahakama na mobile courts hizi zinahitajika ili kuwafikia wananchi. Ni kwa kutambua hilo hivi sasa Mahakama imeshanunua mobile courts sita na zitakapokuwa zimewasili zitapelekwa kwenye maeneo yenye mtawanyiko mkubwa kama Manyoni kwa Mheshimiwa Mbunge ili wananchi walioko maeneo ya mbali waweze kufikiwa, na kadri hali ya fedha itakavyoimarika courts hizo pia zitanunuliwa na maeneo mengine yaweze kufikiwa, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved