Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 5 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 83 | 2024-09-02 |
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kuchimba malambo kwa ajili ya mifugo ili kurahisisha shughuli za ufugaji Mbogwe?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo katika Jimbo la Mbogwe. Aidha, pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali za kujenga mabwawa na kuchimba visima virefu kwa ajili ya maji ya mifugo, bado mahitaji ni makubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kuchimba malambo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe lipo kwenye Mipango ya Serikali. Hata hivyo, kutokana na ufinyu wa bajeti halikuweza kuzingatiwa kuingizwa kwenye vipaumbele vya mwaka 2024/2025. Pamoja na hayo, Serikali inaendelea kuliweka suala hili kwenye mipango ijayo ya utekelezaji wa bajeti kwa kadri ya upatikanaji wa fedha, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved