Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 8 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 131 2024-09-05

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

Ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi – Ndanda

MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-

Je, lini ahadi ya ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi - Ndanda itatekelezwa?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania, imeendelea kuimarisha majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na kukarabati yaliyo katika hali ya uchakavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa mradi wa ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo Chikundi unatekelezwa kwa kutumia bajeti ya mwaka 2024/2025 na mkandarasi yupo eneo la site na ujenzi unaendelea, nashukuru. (Makofi)