Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecil David Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
Ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi – Ndanda MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini ahadi ya ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi - Ndanda itatekelezwa?
Supplementary Question 1
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mhesimiwa Naibu Spika, kwanza nashukuru kwa majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Ni kweli mkandarasi yuko site anaendelea na ujenzi Chikundi na kazi hiyo inaenda kwa kasi sana, naamini ndani ya muda mfupi itakamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo ni kwamba mahitaji ya majengo ya Mahakama ni makubwa. Tunatambua ni maeneo mengi. Hivi sasa Kata ya Lukuledi ambayo inasimamia kwenye Tarafa ya Lisekese wanatoa huduma za Mahakama kupitia Ofisi ya Kata ambayo inamlazimu Hakimu baada ya kutoa hukumu abebe ma-file yake pamoja na documents nyingine na kusafiri nazo zaidi ya kilometa 40 kwenda kuzihifadhi Masasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ione uwezekano wa kujenga jengo la Mahakama kwenye Kata ya Lukuledi ambako tayari eneo lilishatengwa kwa ajili ya Tarafa ya Lisekese. Naipongeza sana Serikali kwa kutekeleza hayo.
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mhehimiwa Naibu Spika, kwanza nashukuru kwa shukrani hizi anazozitoa Mheshimiwa Mbunge na kwa kweli shukrani zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa dhamira safi ameamua kuimarisha sekta ya utoaji haki na haki jinai katika nchi yetu, ikiwa ni pamoja na kuimarisha hii sekta ya Mahakama.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ombi lake juu ya Kata yake ya Lukuledi kule Masasi tutaona uwezekano wakati tunahuisha mpango wa awamu ya pili ya ujenzi na uimarishaji wa sekta ya Mahakama uwezekano wa kuiingiza Mahakama aliyoitaja katika mpango wa ujenzi, ahsante.
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
Ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi – Ndanda MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini ahadi ya ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi - Ndanda itatekelezwa?
Supplementary Question 2
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, katika Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Kiponzelo, Kijiji cha Kiponzelo lipo Baraza la Mkoloni/Baraza la Chifu. Nilishaomba tujengewe Mahakama pale ili tuboreshe huduma za Mahakama, je, ni lini sasa Serikali itazingatia ombi hilo halali? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nilipokee ombi la Mheshimiwa Mbunge, lakini nakiri kwamba Serikali imefanya juhudi ya kuanza kujenga majengo ya Mahakama za Wilaya maeneo ambayo haikuwa nazo, na najua katika Mkoa wa Iringa ni moja ya wilaya zilizonufaika. Sasa hii Kiponzelo aliyoitaja tutaona uwezekano wa kuiingiza katika mpango wa ujenzi tutakapohuisha mkakati wa uimarishaji wa sekta ya Mahakama, ahsante.
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
Ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi – Ndanda MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini ahadi ya ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi - Ndanda itatekelezwa?
Supplementary Question 3
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, uhitaji wa Mahakama za Mwanzo kwenye Tarafa za Kibutuka na Makata, Wilayani Liwale ni mkubwa sana, je, Serikali iko tayari kutimiza ahadi hiyo ya kujenga hizo Mahakama za Mwanzo kwenye Tarafa hizo mbili?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mhehimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, Serikali ina dhamira ya kuendelea kuimarisha utoaji wa haki kwa wananchi kupitia Mahakama yake ikiwa ni pamoja na kupeleka hizi huduma karibu na wananchi. Kwa hiyo, kipaumbele ni kwenye tarafa ambazo hazina kabisa Mahakama zikiwemo hizo za Kibutuka na Makata.
Mheshimiwa Naibu Spika, napokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge kwamba wakati kutekeleza mpango wa awamu ya pili ya ujenzi tarafa alizozitaja Idara ya Mahakama ione uwezekano wa kuziingiza katika mapngo wa ujenzi, nashukuru.
Name
Nashon William Bidyanguze
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Kusini
Primary Question
Ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi – Ndanda MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini ahadi ya ujenzi wa Mahakama Kata ya Chikundi - Ndanda itatekelezwa?
Supplementary Question 4
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba niulize swali kwamba ni lini Mahakama ya Mwanzo ya pale Buhingu itajengwa?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mhehimiwa Naibu Spika, naomba tu nipokee ombi la Mheshimiwa Mbunge juu ya kujenga hii Mahakama ya Mwanzo kwa sababu kama nilivyosema kwenye majibu ya Waheshimiwa Wabunge kwenye maswali yao ya nyongeza, kipaumbele tulianza na Mahakama Jumuishi ngazi ya mikoa. Tumeingia ngazi ya wilaya kuhakikisha kwamba wilaya zote zinapata Mahakama na sasa tunashuka kwenda kwenye Mahakama za Mwanzo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kadiri hali ya fedha itakavyoruhusu na kwa mazungumzo yetu na wadau wa maendeleo Mahakama ya Mwanzo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge kule Mkoani Kigoma itazingatiwa, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved