Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 8 Finance and Planning Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 133 2024-09-05

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

Ununuzi wa Meli Nane za Uvuvi

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:-

Je, lini Serikali itanunua meli nane za uvuvi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020 – 2025?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ununuzi wa meli nane za uvuvi kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM wa mwaka 2020, Ibara ya 43(b) unaendelea kupitia Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) meli nne na Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO) meli nne. Aidha, kati ya meli nne za TAFICO, Shirika limeanza na ununuzi wa meli mbili za awali za uvuvi wa bahari kuu kutumia mishipi (long line fishing vessel). Meli hizi zitanunuliwa na Serikali, kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kwa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo (IFAD).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa meli mbili za awali hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kama ifuatavyo:-

(i) Kukamilika kwa msawazo (specification) za meli mbili zenye urefu wa meta-39.9;

(ii) Kukamilika kwa Tathmini ya Athari za Mazingira na Kijamii za Uvuvi wa Bahari Kuu;

(iii) Kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa awali (pre - feasibility study) na upembuzi yakinifu kamili (full feasibility study) wa ununuzi na uendeshaji wa meli; na

(iv) Kwa sasa maandalizi ya nyaraka kwa ajili ya kutangaza zabuni yanaendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.