Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

Ununuzi wa Meli Nane za Uvuvi MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itanunua meli nane za uvuvi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020 – 2025?

Supplementary Question 1

MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na naipongeza Serikali kwa majibu, lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Ilani imeelekeza kwamba ununuzi wa meli hizi ni kwa kuzingatia pande mbili za Muungano na Mheshimiwa Waziri amesema kuna mchakato wa ununuzi wa meli mbili.

Je, Zanzibar inakwenda kunufaika vipi kutokana na ununuzi wa meli hizo mbili za awali?

Swali la pili, je, kuna ushirikiano gani kati ya ZAFICO na TAFICO katika ununuzi wa meli hizo?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hili la kwanza, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua Zanzibar inanufaika vipi?

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi meli ziko nane na meli hizi zimegawanywa katika pande zote mbili, Bara meli nne na Zanzibar meli nne. Kama nilivyosema kupitia TAFICO tayari meli mbili zabuni zimeshatangazwa na kwa bahati nzuri sana kule Zanzibar tayari wao walishafika mbali zaidi kwenye mchakato wa manunuzi wa meli hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kupitia taratibu za kimanunuzi Zanzibar wao wanaendelea na utaratibu wao na kwa sababu tulishagawana meli hizi na huku Bara nao wanaendelea na utaratibu wao. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba meli hizi zitakaponunuliwa pande zote mbili zitanufaika na manunuzi ya meli hizi na kila kitu kitakwenda sawa sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uhusiano kati ya ZAFICO na TAFICO, mashirika haya ni ya umma, yanashirikiana katika kubadilishana utaalam, kufanya utafiti na mambo mengine, lakini kazi kwa maana ya kazi hizi za uvuvi na shughuli zote zinazohusiana na masuala ya uvuvi ushirikiano wa mashirika haya ni mkubwa na wanashirikiana kwa karibu sana, ahsante.

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

Ununuzi wa Meli Nane za Uvuvi MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itanunua meli nane za uvuvi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020 – 2025?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, hivi tunavyoongea kuna sintofahamu kwenye ukanda wote unaozunguka Ziwa Victoria hasa Visiwa vya Ukerewe kwamba kuanzia sasa muda wowote Ziwa Victoria litafungwa.

Je, Serikali inaweza kutoa kauli kuondoa sintofahamu hii kwa wananchi hasa wa visiwa vya Ukerewe? Nashukuru. (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, hii sintofahamu ya kufunga ziwa sijajua wanaitoa wapi, kwa sababu wako wataalamu wa propaganda wanatengeneza maneno wanayasambaza kwa wavuvi kuleta taharuki. Serikali mpaka sasa haina mpango wowote wa kufunga Ziwa Victoria mpaka hapo itakapokuwa imesema baadaye. Kama kutakuwa na umuhimu wa kufunga Ziwa Victoria, Serikali itafuata michakato yote na taratibu zote kuanzia chini mpaka juu ili maamuzi ya kufunga ziwa yawe ni maamuzi ya wote na siyo maamuzi ya mtu mmoja, ahsante. (Makofi)