Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 9 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 108 2024-04-18

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:-

Je, wahitimu wangapi wa vyuo wanafanya kazi ya kujitolea na wangapi wameajiriwa na kujiajiri baada ya kujitolea?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilianza rasmi kuratibu utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Mafunzo ya Uzoefu wa Kazi kwa Wahitimu (internship) mwaka wa fedha 2019/2020. Tangu kuanza utekelezaji wa programu hii, jumla ya wahitimu 21,280 wamenufaika, ambapo wanaume ni 11,281 na wanawake ni 9,999. Miongoni mwa wanufaika hao, jumla ya wahitimu 3,772 wamepata kazi, wanaume wakiwa ni 2,265 na wanawake ni 1,507.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kuna wengine wanaajiriwa Serikalini, sekta binafsi na nje ya nchi, lakini kazi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuwaongezea uwezo.