Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 53 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 686 | 2024-06-25 |
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga malambo ya kuhifadhia maji ya kunyweshea mifugo katika Kata za Miguruwe, Samanga, Tingi, Njinjo na Mitole?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuwekeza katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya maji ya mifugo ili kutatua changamoto kubwa iliyopo ya upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali za kujenga malambo na kuchimba visima virefu kwa ajili ya maji ya mifugo, bado mahitaji ya miundombinu ya maji kwa mifugo ni makubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya upatikanaji wa maji ya mifugo katika Kata ya Miguruwe, Samanga, Tingi, Njinjo na Mitole katika Jimbo la Kilwa Kaskazini na imeshaweka maombi haya kwenye vipaumbele vya Wizara ili yajumuishwe katika mpango wa Bajeti ya Wizara ya mwaka 2025/2026 kulingana na upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved