Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga malambo ya kuhifadhia maji ya kunyweshea mifugo katika Kata za Miguruwe, Samanga, Tingi, Njinjo na Mitole?
Supplementary Question 1
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha huduma ya malisho katika Wilaya za Kilwa, Nachingwea na Liwale Mkoani Lindi ili kutatua changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ningependa kujua, kwa kuwa Serikali haijawahi kuitisha kongamano lolote la Kitaifa kwa kuwashirikisha Waheshimiwa Wabunge katika kutatua changamoto ya wakulima na wafugaji. Je, ni lini itaitisha kongamano hili ili tuweze kutatua changamoto hii ambayo inakabili Taifa kwa sasa? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali kwa sasa kuhusiana na kuongeza malisho nchini tayari tumekwishatangaza na siku ya Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ninadhani mlimwona Mheshimiwa Waziri. Alikuja na mbegu ambazo ziko tayari kusambazwa kwa nchi nzima kwa ajili ya kuwagawia wafugaji waweze kuzalisha mbegu kwa ajili ya mifugo yetu katika maeneo yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mbegu hizo ziko tayari. Huo ndiyo mkakati namba moja, kuongeza malisha ambayo yatasaidia wafugaji wetu katika maeneo hayo. Tuna aina nyingi sana za mbegu zaidi ya aina tano ambazo mfugaji akizipanda zina uwezo wa kujiotesha na kuzaliana na kuzaliana katika maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tuko tayari kupeleka kwenye jimbo lako Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo tumeshaanza kupeleka katika maeneo mengine ya nchi hii, mbegu za malisho ambazo zitatusaidia kupunguza sana kelele hizi za wafugaji na wakulima katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili la pili la kongamano, Mheshimiwa Mbunge tumelichukua tutakwenda kulifanyia maandalizi na mara litakapokamilika tutawaletea taarifa ili tuweze kupata elimu ya pamoja, wataalamu watatupatia elimu ya pamoja sisi Wabunge ili tuweze kupata ...
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga malambo ya kuhifadhia maji ya kunyweshea mifugo katika Kata za Miguruwe, Samanga, Tingi, Njinjo na Mitole?
Supplementary Question 2
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante; kwa kuwa mtu ni afya lakini pia hata mifugo inahitaji afya bora ikiwa ni pamoja na kuoga, chanjo na matibabu. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho ili ng’ombe wetu nao waweze kuoga na kuwa na afya njema, kwenye Kata ya Shabaka, Mwingiro, Kaboha, Izunya yakafika na Bukwimba? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli anachosema Mheshimiwa Mbunge na hiyo ndiyo sababu ya mifugo yetu inakosa sifa ya kwenda kuuzwa nje ya nchi kwa sababu haifuati utaratibu unaotakiwa wa Kimataifa. Ndiyo maana Serikali imekuwa ikihamasisha sana mifugo hii iweze kuoshwa katika maeneo mbalimbali na mpango wa Serikali ni kujenga majosho kwa wafugaji wote wanakopatikana ndani ya nchi yetu. Tuko tayari kuja kwenye maeneo hayo aliyoyasema Mheshimiwa Mbunge, kuona kama kuna uwezekano wa kujenga majosho ili mifugo hii iweze kupata hiyo huduma. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved