Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 3 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 40 | 2024-08-29 |
Name
Ali Juma Mohamed
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shaurimoyo
Primary Question
MHE. ALI JUMA MOHAMED: aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuharakisha malipo ya wastaafu nchini?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ali Juma Mohamed, Mbunge wa Shaurimoyo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Mpango wa Serikali uliopo kwa sasa ni pamoja na mipango ifuatayo katika kuhakikisha kwamba mafao yanalipwa kwa wakati:-
(i) Kuharakisha malipo kwa kupunguza muda wa kuchakata malipo hayo ambapo kwa sasa malipo yanalipwa chini ya siku 60 na imetungwa kabisa sheria ya kuweza kuhakikisha ndani ya siku 60 malipo yanafanyika;
(ii) Kutumia mfumo wa TEHAMA mfano PSSF Kiganjani ambapo mtumishi anapata taarifa za muda wote na hivyo kujua hali ya michango yake; na
(iii) Kupunguza mrundikano wa madai kwa kulipa madeni ya zamani mfano yale ya kabla ya mwaka 1999 ambapo mwaka 2012 Serikali ililipa zaidi ya trilioni mbili na pia michango ya wanachama kulipwa moja kwa moja kupitia Hazina kwenda katika Mfuko.
Mheshimiwa Spika, mwisho, marekebisho ya sheria mbalimbali yamefanyika yakiwemo sheria ambayo tutaiwasilisha hapa Bungeni kwa siku ya leo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved