Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 3 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 44 | 2024-08-29 |
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza:-
Je, upi uwiano wa mwalimu na mwanafunzi nchini?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, uwiano wa mwalimu na wanafunzi kwa shule za msingi mwaka 2024 ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 64 (1:64). Aidha, kwa upande wa shule za sekondari mahitaji ya walimu yanazingatia idadi ya masomo yaliyopo katika shule husika ambapo mwalimu anatakiwa kufundisha masomo yasiyozidi mawili na vipindi visivyozidi thelathini kwa wiki katika mkondo mmoja wenye wanafunzi 40.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa shule za sekondari hakuna uwiano halisi wa jumla kwa mwalimu na wanafunzi kwa masomo yote kwa kuwa kila somo lina idadi ya vipindi tofauti na somo lingine. Serikali imekuwa ikifanya jitihada kuajiri walimu wa elimu ya msingi na sekondari ili kupunguza tatizo la upungufu wa walimu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved