Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 5 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 71 | 2024-11-04 |
Name
Charles John Mwijage
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Primary Question
MHE. CHARLES J. MWIJAGE aliuliza:-
Je, lini Barabara ya Kata ya Rutoro itajengwa kwa kuwa maombi yalishawasilishwa TARURA?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilifanya usanifu kwa kiwango cha changarawe kwa barabara za Kata ya Rutoro zenye jumla ya kilomita 67.6 ambazo zimekisiwa kugharimu shilingi bilioni 8.078. Aidha, katika mwaka 2023/2024, Serikali imetumia shilingi milioni 445 kwa ajili ya ufunguaji na matengenezo ya barabara ya Kishuro - Mishambya katika Kata ya Ngenge, yenye urefu wa kilomita 13 kwa kiwango cha changarawe pamoja na ujenzi wa makalavati 44 ambayo yamekamilika na madaraja madogo matatu ambayo yako hatua za mwisho za ukamilishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuzipa kipaumbele barabara za Kata ya Rutoro ili zifunguliwe na kupitika kwa kipindi chote kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved