Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 6 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 103 2024-11-05

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:-

Je, lini minara itajengwa vijiji vya Kata ya Bwawani na Vijiji vya Nengung’u, Oloitushula, Olchorovus, Engutukoit, Losinoni Juu na Losinoni Kati?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imekamilisha utekelezaji wa ujenzi wa minara mitano ya kufikisha mawasiliano ya simu katika Kata za Oljoro, Olmotonyi na Oldonyosambu zilizopo Wilayani Arumeru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini katika Vijiji vya Kata ya Bwawani na Vijiji vya Nengung’u, Engutukoit, Losinoni Juu na Losinoni Kati ili kubaini mahitaji halisi ya huduma za mawasiliano katika kata hizo na kuweka mkakati wa namna bora ya kufikisha huduma za mawasiliano hitajika.