Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Noah Lemburis Saputi Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:- Je, lini minara itajengwa vijiji vya Kata ya Bwawani na Vijiji vya Nengung’u, Oloitushula, Olchorovus, Engutukoit, Losinoni Juu na Losinoni Kati?
Supplementary Question 1
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nitakuwa na maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa wananchi wa Kata ya Bwawani na Vijiji vya Nengung’u, Oloitushula, Olchorovus, kwa maana ya Kata ya Musa na Engutukoit, Losinoni Juu na Losinoni Kati, kwa maana ya Kata ya Oldonyosambu hawana mawasiliano, je, ni lini sasa Serikali itakwenda kuanzisha mradi huu kupitia UCSAF ili wananchi hawa wanaoteseka na mawasiliano waweze kuwa na mawasiliano? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kufika katika maeneo haya, akapige simu ili ajionee changamoto hii wanayoipata wananchi? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Noah, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipende kukupongeza sana Mheshimiwa Noah kwa namna ambavyo umeendelea kufuatilia suala hili. Tumeshaongea mara nyingi, lakini naomba nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwa sababu kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi tayari wataalamu wetu wa UCSAF watakwenda kufanya tathmini. Hivyo mara baada ya ukamilishaji wa tathmini hii nikupe matumaini kwamba shughuli hii itaanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutembelea eneo hili lenye tatizo la mawasiliano nipo tayari. Baada ya Bunge Mheshimiwa Mbunge tutawasiliana namna njema ya kwenda kufika katika eneo hili. (Makofi)
Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:- Je, lini minara itajengwa vijiji vya Kata ya Bwawani na Vijiji vya Nengung’u, Oloitushula, Olchorovus, Engutukoit, Losinoni Juu na Losinoni Kati?
Supplementary Question 2
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Kijiji la Elerai katika Kata ya Olmolog, Wilayani Longido, wana changamoto kubwa ya mawasiliano. Je, ni lini Serikali itakamilisha ahadi yake ya kujenga mnara? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nimpongeze Mheshimiwa Zaytun Swai kwa swali lake na ufuatiliaji na yeye ni miongoni mwa Wabunge wanaofuatilia sana maeneo haya ya Longido. Nikutoe hofu Mheshimiwa Zaytun, kijiji hiki ulichokitaja na katika kata hii hapa Longido na yenyewe wataalamu wetu wanaendelea kuhakikisha mawasiliano yanapatikana ya uhakika wakati wote. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved