Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 55 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 709 2024-06-27

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: -

Je, Serikali ina mikakati gani ya kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji yanayotokea kwenye jamii kwa sababu za wivu wa kimapenzi?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inayo mikakati mbalimbali inayolenga kutokomeza ukatili dhidi ya watoto hapa nchini, mikakati hiyo pamoja na:-

(i) Kuboresha vituo vya huduma kwa wateja ili kuwawezesha wananchi kupata elimu na kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa wakati;
(ii) Kutoa huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa jamii na kutoa hifadhi ya dharula kwa manusura wa vitendo vya ukatili;

(iii) Kuratibu Madawati ya Jinsia katika maeneo ya umma na kuwawezesha wananchi kiuchumi;

(iv) Kuimarisha uendeshaji, usimamizi na uratibu wa mabaraza ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa.

Mheshimiwa Spika, mikakati hiyo imebainishwa katika Mpango Kazi wa Taifa wa Pili wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto pamoja na Sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2023 kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji yanayotokea kwenye jamii kwa sababu za wivu wa kimapenzi.

Mheshimiwa Spika, ni pamoja na kuboresha vituo vya huduma kwa wateja, ili kuwawezesha wananchi kupata elimu na kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa wakati, kutoa huduma za afya ya akili na msaada wa kisakolojia kwa jamii. Kutoa hifadhi ya dharura kwa manusura wa vitendo vya ukatili, kuratibu madawati ya jinsia katika maeneo ya umma na kuwawezesha wananchi kiuchumi, kuimarisha uendeshaji, usimamizi na uratibu wa mabaraza ya usuluhishi na migogoro ya ndoa.

Mheshimiwa Spika, mikakati hiyo imebainishwa katika Mpangokazi wa Taifa wa pili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na Sera ya Jinsia ya Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2023 kwa lengo la kukubaliana na vitendo vya ukatili, ikiwemo mauaji yanayotokea kwenye jamii kwa sababu ya wivu wa kimapenzi. Ahsante.