Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mikakati gani ya kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji yanayotokea kwenye jamii kwa sababu za wivu wa kimapenzi?

Supplementary Question 1

MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo; nimeona mikakati ya Serikali na ni mizuri, lakini sijaona mkakati wa kuishirikisha jamii yenyewe katika ulinzi dhidi ya vitendo vya udhalilishaji. Sasa, je, Serikali haioni haja ya kuishirikisha jamii moja kwa moja katika ulinzi dhidi ya vitendo hivi kama ambavyo wanafanya wenzetu wa Jeshi la Polisi katika dhana ya ulinzi shirikishi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa, vitendo hivi kwenye jamii vinatokea mara nyingi, Watanzania wenzetu wanapoteza Maisha. Je, Serikali haioni haja ya kushirikiana na viongozi wa dini katika kuwapa elimu wananchi kwa sababu, vitendo vinasababishwa na mmong’onyoko wa maadili vilevile na hofu ya wananchi kupoteza hofu ya Mungu na wanaojenga hofu ya Mungu na maadili ni viongozi wetu wa dini, sasa Serikali haioni haja ya kushirikisha viongozi wa dini? Ahsante.

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo. Swali lake la kwanza, Serikali imekuwa ikishirikiana na jamii katika kutekeleza afua za ulinzi na usalama katika jamii. Ndiyo maana Kamati zetu zinaanzia katika vijiji, Mwenyekiti wa Kijiji hadi Taifa, ili kuhakikisha kuwapa elimu ya ulinzi na usalama kwa jamii, ili wananchi wawe na uelewa kuhakikisha kwamba, usalama katika nchi unakuwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, Wizara inashirikiana na viongozi wa dini katika kutekeleza Mpango wa Pili, MTAKUWWA, ambao viongozi wa dini wamo katika Kamati ya Ulinzi na Usalama. Kamati hiyo inaanzia Vijijini hadi Taifa kuhakikisha Mpango wa Pili wa Taifa wa MTAKUWWA unakamilisha Sheria na hatua zake na viongozi wa dini kuhakikisha kwamba, wanatoa miongozo na makongamano katika jamii, kutoa elimu ya kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na migogoro ya msongo wa mawazo. Ahsante.

Name

Rose Cyprian Tweve

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mikakati gani ya kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji yanayotokea kwenye jamii kwa sababu za wivu wa kimapenzi?

Supplementary Question 2

MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuwa, vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia vimekuwa vikiongezeka kila mwaka. Sasa, nataka kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri, je, Serikali iko tayari kupitia Vifungu vya Sheria kwa sababu, vimekuwa vikikinzana na kuchochea changamoto hii? Kwa mfano, kijana wa miaka 18 Sheria yetu inamtambua anaweza kuoa na kuolewa na anaweza kupiga kura kwa sababu, anaweza kutambua mazuri na mabaya.

Mheshimiwa Spika, lakini ikija kwenye adhabu, kijana wa miaka 18 na ambaye, yuko chini ya miaka 18 ambaye, amelawiti na kubaka adhabu yake ni siku 30 na kuchapwa viboko. Kwa hiyo nataka kujua, je, mko tayari kufanya mapitio ya hii Sheria? Nakushukuru sana.

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rose. Serikali kwa kushirikiana na Tume ya Kurekebisha Sheria ipo katika hatua za kuendelea kurekebisha Sheria za adhabu. Tutakapokamilisha tutaleta katika Bunge lako Tukufu, ili kuhakikisha Sheria hizo zinapitishwa na adhabu zinazotolewa zinastahiki kwa mtuhumiwa ambaye amefanya vitendo hivyo vya ukatili. Ahsante.

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mikakati gani ya kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji yanayotokea kwenye jamii kwa sababu za wivu wa kimapenzi?

Supplementary Question 3

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ni juzi tu mtoto mwenye ulemavu wa ualbino Sengerema amenusurika na kifo. Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu jambo hili ambalo linaanza kutoa mizizi mikubwa katika nchi yetu? (Makofi)

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA): Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kumjibu Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi kwa kumwambia kwamba, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alitoa taarifa ya Serikali. Serikali imekwishatoa maelekezo kwa Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa yote na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kwamba, wanaimarisha ulinzi na usalama kwa watu wenye ualbino.

Mheshimiwa Spika, lakini tuseme tunaendelea kuwapa elimu Watanzania kuwathamini na kuwajali watu wenye ualbino, ili wasiwadhuru. Sisi tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu jambo hili na tunawataka pia, walezi waendelee kuwa karibu na watoto hawa. Ahsante. (Makofi)