Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 25 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 338 2024-05-14

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaifanyia marekebisho Sheria ya Kifuta Machozi kwa madhara yanayosababishwa na wanyamapori kwani iliyopo inawakandamiza wananchi?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikilipa kifuta jasho na kifuta machozi kama mkono wa pole au faraja kwa wananchi wanaopata madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa lengo la kuimarisha mtazamo chanya kwa wananchi juu ya shughuli za uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori nchini. Malipo hayo yamekuwa yakifanyika kwa mujibu wa Kanuni za Kifuta Jasho na Kifuta Machozi za Mwaka 2011 na kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya mapitio ya Kanuni za Kifuta Jasho na Machozi za Mwaka 2011 kwa lengo la kuboresha viwango vya malipo ya kifuta jasho na kifuta machozi. Aidha, Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushauriana na Wizara ya Fedha kama mdau muhimu katika kufanikisha suala hili, inafanyia kazi viwango vipya vya kifuta jasho na kifuta machozi ili kuviingiza kwenye Kanuni zinazofanyiwa marekebisho.