Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itaifanyia marekebisho Sheria ya Kifuta Machozi kwa madhara yanayosababishwa na wanyamapori kwani iliyopo inawakandamiza wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu yanayotia moyo ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nawapa pole wananchi wa Kata ya Mwangeza kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakiathirika na tembo, lakini bado hawapati huduma inayostahili kutoka Serikali. Swali la kwanza; Serikali haioni kwamba suala hili sasa linapaswa kuletwa kama sheria ili lifanyiwe mabadiliko badala ya kufanyiwa mabadiliko kama Kanuni?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa jambo hili limekuwa likipigiwa kelele na Wabunge humu ndani kila kona. Serikali haioni kwamba, sasa suala hili linapaswa kuletwa kwa hati ya dharura ili Sheria hii ya kifuta jasho itazamwe ambayo inaawaathiri sana wananchi wa Tanzania? Ahsante. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mtinga, yote kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kanuni zinapotumika ni sehemu ya utekelezaji wa sheria. Naomba kurudia, Kanuni zinapotumika ni utekelezaji wa sheria ambazo Bunge hili limezitunga. Ni kweli kwamba, yapo maeneo ambayo Sheria ya Uhifadhi na Sheria ya Wanyamapori imepitwa na wakati, Serikali iko kwenye mchakato wa kufanyia mapitio na kwa kadri muda utakavyokubaliana na vipindi vya Bunge, Serikali itawasilisha marekebisho hayo.