Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 41 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 537 2024-06-05

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina mkakati wa kuongeza uzalishaji wa mpunga katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Bonde la Ibanda kwa kujenga bwawa na miundombinu ya umwagiliaji. Usanifu wa Bonde la Ibanda umekamilika na taratibu za manunuzi za kupata mkandarasi zimekamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatekeleza ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Ibanda kupitia mkandarasi M/S Jiangxi Geo-Engineering kwa mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 13.6 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 21.2 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa.