Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 1

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa mradi huu unahusisha Wilaya mbili, Wilaya ya Sengerema na Wilaya ya Geita, wananchi wa Wilaya ya Geita walishalipwa pesa zao kupisha mradi huu. Je, lini wananchi wa Sengerema watalipwa pesa hizo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, lengo la mradi huu ni kuongeza thamani ya zao la mpunga. Je, kuna mradi gani mwingine ambao unaweza ukajengwa katika eneo hilo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua kwamba kuna madai ya baadhi ya wananchi hususani katika Halmashauri ya Sengerema na sisi kama Serikali tunalifanyia kazi na tutaleta majibu kwa sababu lipo katika mchakato na mimi nitakuwa sehemu ya watu ambao watakwenda kuwaeleza wananchi juu ya faida za huo mradi na wale ambao watapisha na fidia ambayo watalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo hilo ni mradi gani utajengwa? Mradi ni huu huu mmoja isipokuwa tutakwenda kuwaelimisha juu ya aina ya mazao wanayoweza kuyafanya zaidi ya mpunga peke yake, ahsante. (Makofi)

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 2

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, skimu za umwagiliaji maji katika Wilaya ya Bahi miundombinu yake ni chakavu. Nini mkakati wa Serikali wa kurekebisha skimu hizi ili wakulima waweze kupata tija?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba maelekezo tuliyopewa Wizara ya Kilimo na Mheshimiwa Rais ni kurekebisha skimu zote chakavu nchini na kujenga skimu mpya katika mabonde yote yanayohitaji skimu mpya. Kwa hiyo, lipo katika mpango na Bahi ni mashahidi kwamba kuna fedha tumeshapeleka za awamu ya kwanza na tutaleta kwa ajili ya kurekebisha skimu zote ambazo zimebakia.

Name

Munira Mustafa Khatib

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 3

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miaka mitatu sasa Wizara ya Kilimo imekuwa ikitekeleza miradi ya umwagiliaji, lakini miradi hii inaonekana ikisuasua. Je, ni sababu gani miradi hii ya umwagiliaji imekuwa ikisuasua? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumekuwa tukitekeleza miradi mingi na maeneo mbalimbali nchini na kwa sababu ukishakuwa na miradi mingi maana yake mahitaji makubwa ya fedha yanakuwa yanahitajika na wakati mwingine tumekuwa tukichelewa kutoa zile advance payment ndiyo maana unakuta miradi imechelewa na sisi hilo tunakiri kama Wizara, lakini sasa hivi Wizara ya Kilimo tumekaa na Wizara ya Fedha tumekubaliana kuhakikisha fedha zitakuwa zinatoka kwa wakati na wale ambao hawajalipwa watalipwa kwa wakati ili kuhakikisha miradi hii inaisha kwa kadiri ambavyo tumekubaliana kwenye yale makubaliano au mkataba.

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 4

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi, Scheme ya Mangisa imejengwa muda mrefu na imejaa udongo na tuliomba fedha kwa ajili ya kuondoa ule udongo. Je, ni lini Serikali italeta fedha ili scheme ile ikaweze kuwafaidisha na kuwasaidia wakulima wa Mangisa? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba jambo hili na mimi nalifahamu na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inalifanyia kazi. Sehemu ambayo ipo sasa hivi ni kwamba wanatafuta fedha ili kuhakikisha kwamba tunatoa ili iweze kuwasaidia wananchi ule mradi uweze kufanya kazi, ahsante. (Makofi)

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 5

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kitulo ndiyo wanaongoza kwa uzalishaji wa viazi katika Mkoa wa Njombe na sisi kama halmashauri tumejipanga kwamba tunatakiwa tuwawezeshe kuwa na scheme na tulipeleka maombi kwenye Wizara yenu ya Kilimo, kujenga scheme katika Kata ya Kitulo ili uzalishaji wa viazi uongezeke kwa ukubwa na kwa upana wake.

Mheshimiwa Waziri, ni ipi commitment ya Serikali kuwasaidia wananchi wa Kitulo wawe na scheme ya umwagiliaji ili wazalishe viazi msimu wote wa mwaka kwa ajili ya manufaa ya uchumi wao? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, namthibitishia tu Mheshimiwa Mbunge na akawaambie wananchi wa Makate, Kata ya Kitulo kwamba tutajenga hiyo scheme kwa sababu ni sehemu ya miradi mikubwa ambayo ipo katika kipaumbele chetu kama Wizara, ahsante. (Makofi)

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 6

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya umwagiliaji kwenye Kata za Masela na Bukangilija, Kata ya Badi upembuzi yakinifu pamoja na usanifu umekamilika. Je, ni lini Serikali itajenga miradi hiyo ya umwagiliaji? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba Miradi ya Masela na Bukangilija iliyoko Maswa ni kwamba tumeshamaliza upembuzi yakinifu na feasibility study, sasa hivi tuko katika hatua ya kumtafuta mkandarasi ili tuweze kumkabidhi site aanze kazi, ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 7

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, ni lini Scheme ya Kimbande, Mjini Mbamba Bay itawekewa miundombinu ili vijana wengi na hasa wahitimu waweze kunufaika? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba Scheme ya Kimbande iliyopo Nyasa ni kwamba ipo katika mipango ya Serikali na tuko katika hatua za mwisho kuhakikisha kwamba tunatafuta mkandarasi ili ianze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa. (Makofi)

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mpunga Bonde la Ibanda na kiasi gani kinahitajika kuweka skimu ya umwagiliaji?

Supplementary Question 8

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, je Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula katika Bonde la Mto Matandu kupitia scheme za umwagiliaji? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba Bonde la Matandu lililoko katika Halmashauri ya Kilwa ni moja ya bonde ambalo sisi Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tunalifanyia feasibility study ili liweze kufanya kazi kipindi chote kwa kuwa na miundombinu bora na ya kisasa. Kwa hiyo, hilo ndiyo jukumu kubwa ambalo sasa hivi tunalifanya. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tukishamaliza tutakuja na tutazungumza na wananchi na wataona faida ya huo mradi, ahsante. (Makofi)