Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 51 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 659 2024-06-21

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -

Je, Serikali imejipanga vipi kukabiliana na ongezeko la bei ya pembejeo za kilimo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ili kukabiliana na ongezeko la bei ya pembejeo, Serikali imeendelea kutekeleza yafuatayo: -

(i) Kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa mazao yote hapa nchini ili kuwapa unafuu wa bei ya mbolea, kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani;

(ii) Kuratibu ununuzi wa pamoja (Bulk Procurement) wa pembejeo za mazao ya korosho, pamba na tumbaku kwa kuagiza kutoka kwenye chanzo cha uzalishaji;

(iii) Kuhamasisha kampuni za pembejeo kutumia reli kusafirisha pembejeo kwenda mikoani ili kupunguza gharama za usafirishaji;

(iv) Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji wa pembejeo za kilimo nchini ili kupunguza utegemezi wa kuagiza kutoka nje ya nchi;

(v) Kuainisha na kutangaza bei elekezi za mbegu bora kila mwaka ili kudhibiti upandaji holela wa bei za mbegu; na mwisho

(vi) Kushirikisha sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji wa mbegu ndani ya nchi kwa kuingia mikataba ya muda mrefu na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) na TARI ili kuzalisha mbegu bora kwa kutumia mashamba ya Serikali.