Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 9 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 147 | 2024-11-08 |
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Uliwa - Njombe utakamilika?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Kijiji cha Uliwa kipo katika Kata ya Iwungilo inayoundwa na vijiji vya Ngalanga, Iwungilo, Igoma na Uliwa, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) iliijumuisha Kata ya Iwungilo katika mradi wa mawasiliano wa awamu ya pili ‘A’ (2A) ambapo mtoa huduma HONORA (TIGO) alijenga minara katika vijiji vya Iwungilo na Ngalanga inaohudumia vijiji vya Ngalanga, Iwungilo, Igoma na Uliwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia UCSAF ilifanya tathmini katika Kijiji cha Uliwa na kubaini kuwa kulingana na jiografia ya kijiji cha Uliwa ambacho kipo bondeni, minara iliyojengwa awali haifikishi mawasiliano katika kijiji hiki. Hivyo, UCSAF tayari imekijumuisha kijiji hiki katika orodha ya vijiji vitakavyonufaika kupitia mradi wa mawasiliano vijijini utakaotekelezwa katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved