Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Uliwa - Njombe utakamilika?
Supplementary Question 1
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana, ninashukuru kwa majibu ya Serikali na kwa kutambua kwamba kweli Uliwa wana tatizo la mawasiliano, sasa nina maswali mawili.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza kwa sababu kijiji hiki kina mahitaji makubwa yanayotambulika, ni lini sasa Serikali itaanza ujenzi? Kwa sababu nimeuliza hili swali zaidi ya mara tatu hapa na nikahakikishiwa itaingia kwenye Mradi wa Minara 758 lini Serikali itanza ujenzi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili nilitaka kujua kama inaonekana kuingiza kwenye bajeti ya kawaida ya Serikali ambayo ndiyo imesemwa hapa mnara unachuka muda mrefu kujengwa ni kwa nini sasa tusihamishe huu mnara tukauhamishia kwenye Mradi wa Minara 748 kwa sababu sisi tuna mnara moja tu na tunaweza tukafanya switching. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deodatus Mwanyika, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusi lini tuaanza ujenzi, ni jana tu Mheshimiwa Mbunge aliweza kuwasiliana na Mheshimiwa Waziri wetu Mheshimiwa Jerry Silaa na akaunganishwa na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Kaka yangu Engineer Peter Mwasalanda na Engineer Mwasalanda ameshamwagiza engineer anayehusika na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini na tayari anajiandaa kuelekea kwenye Kijiji hiki cha Uliwa kufanya tathmini ili tuone population iliyopo pale Uliwa ili wapate mawasiliano ya uhakika. Ninakupongeza sana Kaka yangu Mheshimiwa Deodatus umefuatilia kweli mara nyingi na sasa tutakuja kulifanyia kazi tumekuelewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, switching ya mnara mmoja kwenda eneo lingine Mheshimiwa Mbunge ninaomba baada ya hapa tukutane tena kama ulivyoongea jana na Mheshimiwa Jerry tutawasiliana na DG Peter lengo ni kuhakikisha tunafanikisha. (Makofi)
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Uliwa - Njombe utakamilika?
Supplementary Question 2
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana Mheshimiwa Rais wetu alisaini Minara 758 lakini hata mimi kwenye Jimbo la Kalenga Vodacom walisaini katika Kata ya Masaka Kijiji cha Kaning’ombe. Kwa kuwa Vodacom wamechelewesha kujenga mnara mpaka sasa hawaoni kufanya hivyo ni kuhujumu juhudi za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea maendeleo Wananchi wa Kalenga? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama Vodacom ndio wanaowajibika kujenga mnara pale sisi kama Wizara hatutaruhusu hujuma yoyote kwa nguvu anazoziweka Mheshimiwa Rais wetu. Nikuhakikishie mnara huu utajengwa na tutausimamia.
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Uliwa - Njombe utakamilika?
Supplementary Question 3
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini mnara wa Msasa uliokuwa katika ile Minara 758 utaanza kujengwa kwa sababu ilisainiwa minara miwili lakini wa Msasa mpaka sasa hivi haujaanza kujengwa?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Magessa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia mnara huu na kama tulivyoongea hapo nje nikuhakikishie nitasimamia utekelezaji huu wa mnara uweze kufanyika na mawasiliano ya uhakika yaweze kupatikana kwa wananchi wa eneo wako unaowakilisha.
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Uliwa - Njombe utakamilika?
Supplementary Question 4
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa nafasi Mungu akubariki.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Kasinde Kata ya Kapele, Kijiji cha Ntungwa Kata ya Mkomba, Kijiji cha Naming’ongo Kata ya Chitete havina mawasiliano kabisa pamoja na vijiji vingine na nimeuliza hii ni mara ya nane hapa Bungeni. Wizara mna mkakati gani wa kutusaidia mawasiliano kwenye Jimbo la Momba? Ahsante!
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Nimpongeze Mheshimiwa Condester kwa swali lake. Pole sana kwa kufuatilia kwa muda mrefu lakini hakuna refu linalokosa ncha nikuhakikishie tutakuja kutekeleza. Vijiji vyote hivi ulivyovitaja tutakuja kutembelea na baada ya hapa nitamwagiza yule Mtendaji wa Nyanda za Juu Kusini aweze kufika pale Momba na lazima tuhakikishe ndani ya mwaka huu wa fedha tuweze kuona nini kinafanyika angalau katika eneo moja. (Makofi)
Name
Hassan Zidadu Kungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Uliwa - Njombe utakamilika?
Supplementary Question 5
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niishukuru Serikali kwa kujenga mnara wa mawasiliano wa simu katika Kata ya Ngapa lakini mawasiliano yale ya simu hayafiki katika Kitongoji cha Ngapa B ama Ngapa Mtoni ambapo kuna wachimbaji wengi sana na wanakosa huduma ya mawasiliano ya simu. Je, Serikali haioni haja ya kwenda kuongeza nguvu katika ule mnara ili uweze kufikisha mawasiliano ya simu Ngapa Mtoni? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la uchimbaji ni eneo muhimu sana katika uzalishaji na Pato la Taifa tupo tayari kuja kuongezea nguvu na wananchi waweze kupata mawasiliano ya uhakika. (Makofi)