Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 48 2024-11-01

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:-

Je, lini Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo zitajengwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya kujenga Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ambapo eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 25,000 limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri na eneo la mita za mraba 25,000 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Mheshimiwa Spika, aidha, halmashauri imeshaandaa na kuwasilisha andiko la jengo la ofisi za halmashauri lenye thamani ya shilingi bilioni 5.75 Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa hatua zaidi.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 Serikali itatenga shilingi milioni 200 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Ahsante.