Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, lini Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo zitajengwa?

Supplementary Question 1

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza maswali; nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza, ninamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu aliyotoa. Swali la kwanza; kutokana na ile hali ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuwa ndani ya majengo ya Halmashauri ya Wilaya. Je, Serikali haioni kuwa, kuna umuhimu wa kujenga haraka sana ili kutenganisha mamlaka hizi mbili? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kutokana na majengo yaliyopo sasa hivi yaliyojengwa mwaka 1974 maana yake ni miaka 50 iliyopita. Je, Serikali haioni kuna umuhimu sasa wa kutujengea majengo ya kisasa? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, kwanza ninamshukuru Mheshimiwa Mbunge amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na uhitaji wa kujenga majengo haya mawili; Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Urambo, pamoja na jengo la halmashauri.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati nzuri Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo, kwa hiyo, lile jengo la ofisi Mheshimiwa Waziri Mkuu amelitumia na sisi tumetoa kipaumbele kuhakikisha kwamba mwaka ujao wa fedha tunaanza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wilaya ya Urambo ili liwe la kisasa na kutoa huduma bora kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, nimhakikishie tu kwamba, jengo la halmashauri litakalojengwa pamoja na jengo la Mkuu wa Wilaya ni majengo ya kisasa na ndio maana ombi la fedha shilingi bilioni 5.75 ni majengo yale ya kisasa ya ghorofa ambayo tunaamini yatatoa huduma bora kwa wananchi. (Makofi)

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, lini Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo zitajengwa?

Supplementary Question 2

MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana. Kwanza ninatoa shukrani nyingi kwa Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutujengea jengo jipya kabisa la halmashauri na ukumbi wa mikutano. Sasa ni lini Serikali itajenga Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka mpango mkakati wa ujenzi wa majengo ya Wakuu wa Wilaya kote nchini na mpaka sasa zaidi ya majengo 127 ya halmashauri pamoja na ofisi za Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya zinajengwa na mpango huu ni endelevu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ni moja ya halmashauri ambazo pia zimewekwa kwenye mpango kwa ajili ya kujengewa majengo ya Wakuu wa Wilaya. Ahsante. (Makofi)